Vipimo
Tikiti la asali (honey melon) 1
Unga wa embe au embe 1
Tangawizi 1 Kijiko
Ndimu 1
Sukari ¼ Kikombe cha chai
Arki rose 2 Matone
Namna Ya Kutayarisha
1. Limenye melon na ulikate kate kisha tia kwenye blender
2. Tia unga wa embe au embe iliyokatwa katwa
3. Kisha tia ndimu iliyokatwa vipande kiasi pamoja na maganda yake
4. Halafu weka sukari
5. Saga vizuri hadi ilainike
6. Mimina kwenye jagi kisha tia matone mawili ya arki rose ukoroge na tayari kwa kunywewa
Kidokezo:
Ukiweka ndimu weka na maganda yake unapata ladha nzuri zaidi.