Friday, December 2, 2016

JIFUNZE KUPIKA BIRIYANI SAFI NA RAHISI YA KUKU


Related image
RECIPE SAFI SANA YA BIRIYANI YA KUKU

MAHITAJI

 ( Chakula hiki kinatosha watu 3 hadi 5 )



 600 gram mchele wa basmati basmati
 1 kuku mzima ( toa ngozi na kata vipande vikubwa kama kwenye picha)
6 Vitunguu umbo la kati
15 gram kitunguu swaumu cha kusagwa
10 gram tangawizi ya kusagwa
3 Nyanya katakat vipande vidogo
3 pili pili mbuzi za kijani 
1 fungu la majani ya Mint 
1 fungu la majani ya Coriander (giligilani)
3 kijiko kidogo cha chai Garam masala
100 gram Yogurt 
1 kijiko kikubwa cha chakula juisi ya limao
3 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya samli
3 kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji

VIUNGO VIZIMA VIZIMA PIA VINATAKIWA:

3 vipande vya mdalasini cinnamon stick
6 vipande vya karafuu
2 vipande vya hiriki ya kijani

KWA KUPAMBIA BIRIYANI YAKO:

Mafuta ya kukaangia
1 kitunguu kata slice
10 vipande vya korosho (Cashew nuts)
15 vipande vya zabibu kavu (Rasins)

JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



1. Loweka mchele kwenye maji kwa masaa 3.
2. Kisha chemsha mchele katika maji, chumvi na 1 kijiko cha garam masala kwa dakika 15, kisha toa mchele wako uchuje na weka pembeni. Wali huu ukiubonyeza kwa mikono utavunjika ingawa utakua haujaiva vizuri. Huu ndio ubora unaotakiwa kwani ukiivisha kabisa utakua umekosea.

3. Safisha kuku na kata katika vipande vikubwa.Kumbuka kukata kata mikato katika nyama ili iweze kuja kuiva haraka.



4. Chukua sufuria kubwa linaloweza kuingia mchele na kuku yoote wakati unapika. kisha weka samli iyeyuke
5.  Kisha weka viungo vyoote na kaanga mapaka upate harufu nzuri (aroma).
6. Kisha weka kitunguu na chumvi. Pika mapaka vitunguu vilainike. Kisha punguza moto uwe wa wastani.


7. Kisha weka kitunguu swaumu na tangawizi kaanga mpaka upate rangi ya kahawia.
8. Kisha weka nyanya na pili pili mbuzi. Acha mchanganyiko huu uive mpaka nyanya ipondeke .



9. Kisha weka majani ya mint na coriander . Funika na mfuniko na pika kwa dakika 10.



10. Kisha weka yogurt na unga wa garam masala.
11. Kisha ongeza limao juice na chumvi kidogo.


12.   Kisha chukua vipande vya kuku na weka katika mchanganyiko wako katika sufuria, funika na uache inaendelea kuiva.



13.   Kisha chukau wali na weka juu ya mchanganyiko wako wa kuku na mchuzi
14. Kisha mwagia maziwa juu ya wali.

15. Funika sufuri a yako hakikisha inafunika kabisa mvuke usitoke nje.
16. Baada ya hapo weka moto uwe mkali kabisa kwa dakika 2. KIsha punguza moto na acha ichemke kwa dakika 45.
17. Wakati huo huo pasha moto kikaango ili uweze kukaanga vitu utkavyopambia.




18. Choma vitunguu katika mafiuta mpaka upate rangi ya kahawia.
19. Kisha kaanga korosho mpaka rangi ya kahawia.
20. Kisha kaanga zabibu kavu kwa dakika 1 tu.
21. Baada ya kusubiri kwa dakika 45 sasa zungusha wali wako pamoja na nyama ya kuku vichanganyike pole pole.



22. Pakua chakula chako na ukipambe kisha mpatie mlaji kikiwa cha moto.

MBINU ENDAPO UNATAKA KUTUMIA NYAMA TOFAUTI:
1.Kama unataka kutumia nyama ya ngombe au ya mbuzi au yakondoo.

Unatakiwa nyama uiwekee viungo hivi na ikae usiku kucha katika friji ili iweze kua laini ( 100 gram yogurt, 1 kijiko cha chakula white vinegar- 1 kijiko cha chai garam masala powder).
Kwa mtindo huu wali itabidi upike kwa dakika 10 pembeni.
Katika sufuria ya mchanganyiko wa nyama kwa kufata hatua zile ziule kitakachoongezeka ni muda wa kupika ikiwa ni nyama pika kwa saa 1 na dakika 15.




CHAKULA HIKI NI KITAMU SANA NA NIRAHISI KUKITENGENEZA WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE CHAKULA HIKI.

Tuesday, November 15, 2016

Mapishi ya Chapati za maji



Mahitaji

  • Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo)
  • Yai (egg 1)
  • Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai)
  • Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai)
  • Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai)
  • Maji kiasi
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni  katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari

NAMNA YA KUTENGENEZA MAANDAZI



Chukua Amira ya chenga gram 11



Chumvi nusu kijiko kidogo cha chai


Sukari gram 250


Unga wa ngano kilo moja

Maji ya uvugu vugu nusu lita



Mafuta ya kupikia lita 2 na nusu

Weka pakiti ndogo ya amira yenye ujazo wa gramu 11 yoote kwenye unga wako wa kilo moja



Kisha weka chumvi nusu kijiko kidogo cha chai chumvi hii husaidia kupunguza mafuta ndai yaa andazi baada ya kuiva andazi lako litakua halina mafuta safi na salama kwa mlaji

Weka sukari gram 250 katika unga wako


Baada ya hapo weka mafuta ya moto ujazo wa kikombe kidogo cha chai au gr 250
 changanya vizuri mafuta bado yakiwa yamoto


Kisha weka maji ya uvuguvugu ili kuuwa ngano nakufanya amira kuweza kumuka haraka



Kanda mchanganyiko wako safi kwa kutumia nguvu na umakini mpaka mchanganyiko wako uwe laini


Mchangyanyiko wako kama uko bado ni teketeke na ulizidisha maji kidogo weka unga kiasi kisha endelea kukanda mpakja uwe mkavu na laini

Hapa safi sasa


 Shepu vizuri tayari kwa maandalizi ya kusukuma na kukata 



Sukuma unga wako mpaka saizi ya unmene halisi wa andazi lako utakavyopenda liwe

Kisha tumia kitu chechote kile kukatia kwa umbo lolote lile utakalo lipenda



Yaache kwa muda wa dakika 10 baada ya kuyakata yaumuke kisha itakua tayari kwa kuyachoma


Baada ya kukata maumbo mazuri ya duara unga unaobakia unaweza viringisha maumbo tofauti kama uonavyo katika picha pia unaweza tengeneza hata herufi

 Pasaha mafuta yako katika moto wa wastani yasiwe na moto mkali utapelekea maandazi yako kuungua kisha yaweke katika moto na geuza kila mara ili yasivimbe upande mmoja na ikawa vigumu kuyageuza




Hili ni anfazi lako safi limeshaiva na halina mafuta ndani na safi kabisa

Wednesday, October 12, 2016

Jinsi Ya Kutengeneza Juisi Ya Melon Na Embe




Vipimo


Tikiti la asali (honey melon)                       1

Unga wa embe au embe                            1

Tangawizi                                                 1 Kijiko

Ndimu                                                      1

Sukari                                                      ¼ Kikombe cha chai

Arki rose                                                   2 Matone



Namna Ya Kutayarisha


1.     Limenye melon na ulikate kate kisha tia kwenye blender
2.     Tia unga wa embe au embe iliyokatwa katwa
3.     Kisha tia ndimu iliyokatwa vipande kiasi pamoja na maganda yake
4.     Halafu weka sukari
5.     Saga vizuri hadi ilainike
6.     Mimina kwenye jagi kisha tia matone mawili ya arki rose ukoroge na tayari kwa kunywewa

Kidokezo:

Ukiweka ndimu weka na maganda yake unapata ladha nzuri zaidi.

JINSI YA KUTENGENEZA KEKI YA MAZIWA


Vipimo
Siagi                                                               Kikombe 1
Sukari                                                             Kikombe 1 
Unga                                                               Vikombe 2 
Maziwa                                                           1/2 (nusu) Kikombe 
Mayai                                                              4
Baking Powder                                                1 Kijiko cha supu
Arki rose                                                           kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1.                      Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2.         Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.
3.                       Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.
4.                       Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5.                       Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6.                       Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.
7.                       Ipike (Bake ) mpaka iwive.
8.        Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.